Umoja wa Ulaya (EU) umetangaza kifurushi cha nane cha vikwazo dhidi ya Urusi ambacho kinalenga kuzuia uingizwaji na uuzaji wa bidhaa zinazo zalishwa Urusi kama sabuni, manukato na hata bushashi ‘toilet paper!
Mpango huo unalenga kuinyima Moscow mapato ya biashara kutokana na mzozo wa Ukraine. EU imependekeza kupiga marufuku uagizaji wa bidhaa za usafi zinazotengenezwa nchini Urusi, kutoka sabuni na vitu vya kunyoa hadi karatasi za chooni (bushashi) a deodorant.
Furushi hilo la nane la vikwazo dhidi ya Urusi, lilizinduliwa Brussels siku ya Jumatano, pia litapiga marufuku uagizaji wa bidhaa kadhaa za chuma na kujaribu kuweka kikomo cha bei kwa mafuta ya Urusi.
“Hatukubali kura ya maoni ya uwongo na aina yoyote ya unyakuzi nchini Ukraine, na tumedhamiria kuifanya Kremlin kulipia ongezeko hili zaidi,” Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen alitangaza mini Brussels. Kwa mujibu wa Leyen, kifurushi kilichopendekezwa cha vikwazo kinatarajiwa kuinyima Urusi “mapato ya ziada ya euro bilioni 7 (Sh trilioni 15.8).”
Mpango huo unawahitaji wakazi wa Umoja wa Ulaya kufanya kazi bila bidhaa za “urembo au za kujipodoa” zilizotengenezwa nchini Urusi, vifaa vya kunyoa, “viondoa harufu,” uzi wa meno, sabuni, na karatasi za chooni, mtandao wa Politico umeripoti Alhamisi.