Michezo

Ulipitwa na matokeo ya michuano ya ligi ya Europa? Nimekusogezea hapa

on

everton_3238696kMechi kadhaa zimechezwa jana usiku viwanja mbalimbali katika michuano ya ligi ya Europa, timu kadhaa zilishuka dimbani katika hatua ya 16 bora, katika mechi hizo timu ya Everton ya England imetupwa nje ya mashindano hayo baada ya kubebeshwa bao 5-2 dhidi ya Dynamo Kiev ya Ukraine na kufanya matokeo ya jumla kuwa ni 6-4 kutokana na matokeo ya 2-1 ambayo Everton ilishinda mechi ya kwanza.

Europa

Kwa upande wa timu ya AS Roma imejikuta ikiangukia pua baada ya kufungwa goli 3-0 nyumbani baada ya kucheza na Fiorentina, timu zote kutoka nchini Italy, kwa matokeo hayo Roma imetupwa nje kwa jumla ya mabao 4-1 baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo wao awali.

Nayo Inter Milan ikakwaa kisiki baada kufungwa goli 2-1 dhidi ya Wolfsburg ya Ujeruman na kutolewa kwenye mashindano hayo kwa magoli 5-2 baada ya awali kufungwa mabao 3-1, huku Villarreal ikichapwa goli 1-2 dhidi ya Sevilla na kutolewa nje kwa goli 5-2 ambapo mechi ya kwanza walifungwa goli 3-1.

Ueropa

Mashindano hayo ya Europa kwa sasa yanaingia katika hatua ya robo fainali.

Hautopitwa na stori yoyote inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia twitter instagram na facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza >>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments