Michezo

Hii ni story ya majonzi kwa wapenzi wa soka hasa Klabu ya Everton

on

reading-fans-crying-relegation_1085135
Hii ni habari ni habari ya majonzi kwa mashabiki wa soka duniani hasa wa klabu ya Everton na uongozi mzima kuhusu aliyekuwa rais wa heshima wa klabu hiyo Sir Philip Carter.

Carter ambaye ni mmoja wa waasisi wakubwa ambao waliisaidia timu hiyo hadi kufikia ilipo, kingine kilichoripotiwa leo kinahusu msiba wa Rais huyo ambaye alifariki akiwa na umri wa miaka 87  ambapo amefariki akiwa nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mfupi.

eva

Sir Philip Carter

Rais huyo alikua mmoja ya mashabiki wa timu hii tangu akiwa mtoto ambapo mwaka 1973 alijiunga na timu kama mkurugenzi na mwaka 1978 akawa Mwenyekiti.

Wakati wa uongozi wake kama mwenyekiti akiwa na meneja wake Howard Kendall, Everton ilishinda mataji ya FA cup mwaka 1985 na 1987, 1984 na Kombe la Ulaya 1985.

Alichaguliwa kuwa Raisi wa heshima wa maisha wa timu ya Everton mwaka 2004.

Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenyeTwitter,Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>>  Twitter InstaFB  na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.

Tupia Comments