Breaking News

BREAKING: Maamuzi mapya ya Mahakama Kuu kesi ya Wabunge 8 waliofutwa CUF

on

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam leo August 4, 2017 imetupilia mbali pingamizi la Wabunge 8 wa  Viti Maalumu waliofutwa uanachama na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Prof. Ibrahim Lipumba ya kutaka wabunge wateule 8 wasiapishwe na Bunge.

Uamuzi huo, umetolewa na Jaji Lugano Mwandambo ambaye amesema ametupilia mbali pingamizi hilo la zuio la kuapishwa kwa Wabunge hao 8 na kwa mantiki hiyo, Wabunge wapya walioteuliwa kuziba nafasi zao wanaweza kuapishwa.

Aidha, sababu aliyoitumja Jaji Lugano ni kutokuwepo kwa kifungu sahihi ambapo kunayafanya maombi hayo yasiwe sahihi Mahakamani.

Play kwenye video hii kushuhudia Wanachama wa CUF walivyopigana ndani ya Mahakama Kuu…

Soma na hizi

Tupia Comments