Katika kuhakikisha Wafanyabishara na Wasafirishaji vijijini wanaondokana na mafuta ya kupima kwenye makopo Mamlaka ya usimamizi wa Nishati ya Mafuta na Maji Nchini EWURA imetunga Sheria na kanuni ambayo imeruhusu Mtu yoyote kujenga kituo cha Mafuta Maeneo ya vijijini na kuuza mafuta kwa kwa bei elekezi
Hayo yamesemwa na Meneja EWURA Kanda ya Ziwa George Mhina Mjini. Geita katika kongamano na Taasisi mbalimbali za Serikali zinazo husika na utoaji wa leseni kwa Wafanyabishara na wachimbaji wa Madini.
Mhina amesema kwa Sheria ya Sasa ujenzi wa kituo Cha kuuzia Mafuta vijijini Mtu anaruhusiwa kujenga kwa Shillingi Million 50 lengo likiwa ni kutokomeza Mafuta ya kupima kwa Makopo.
“Wananchi changamkeni fursa ya Ujenzi wa vituo hivyo Ili kutomeza Uuzwaji wa Mafuta kwenye Maeneo yasio rasmi haswa Barabarani na kwenye madumu” Amesema Mhina.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Ndg.Exaudi Kigahe akiwa katika ufunguzi wa Semina kwa wadau wa Mafuta pamoja na wachimbaji wa Madini Mkoani Geita amezitaka Taasisi kuhakikisha zinawasaidia wananchi katika kubuni na kutatua changamoto zao .
Amesema Serikali itaendelea kuwasimamia wananchi wake katika kuondokana na changamoto ambazo wamekuwa wakikumbana nazo huku akitoa Maagizo kwa Taasisi za Serikali kuhakikisha zinatatua kero za wananchi pamoja na Wadau wa Mafuta.