Burudani

Mfahamu mpishi maarufu duniani aliewahi kumuhudumia Ben Pol, Pogba na wengineo

on

Kwa majina kamili anaitwa Nusret Gòkçe maarufu kama Salt Bae umaarufu wake umekuja baada ya ukataji wa nyama ama style ya kipekee anayoitumia  kwenye migahawa yake hasa katika uandaaji wa nyama.

Salt Bae mwenye asili ya Uturuki ana jumla ya migahawa mitano iliyopo kwenye nchi tofauti na hii ndio miji inayopatikana migahawa yake ikiwemo In Mykonos, Miami, New York, Abu Dhabi, pamoja na huko Istanbul, bei yake nyama inategemea na mji au nchi uliyofika katika mgahawa wake kwani zinatofautiana sana

Salt Bae mpaka sasa ameshawahudumia mastaa wakubwa wakiwemo kama Pogba,Beckham, Lukaku, Neymar, Messi, Drake, Dj Khaled,Kibongo bongo ameshawahi kumuhudumia msanii wa Bongo Fleva Ben Pol akiwa na mpenzi wake huko Abu Dhabi.

Kwa mwaka huu alipata shavu la kuonekana katika video ya Dj Khaled iitwayo You Stay ikimuonesha akiandaa nyama.

Nyama anayoandaa na kukuandalia kwenye mgahawa wake unaambiwa inagharimu zaidi ya dolla 500 za kimarekani na kuendelea ambayo ni sawa na fedha za kitanzania Milion

Tupia Comments