Mwimbaji Jux anaye-trend na goma jipya la ‘I LOVE YOU’ kwa sasa, amesema hajafurahishwa na kitendo cha Mwimbaji Harmonize kumuweka bila taarifa kwenye bango lenye majina ya watakao-perform kwenye show yake ya Afro East Carnival tarehe 5 March 2022.
Kwenye Interview na Amplifaya ya Clouds FM Jux amesema ———> “Ni muda Harmonize aliniandikia msg ya kutaka niwepo kwenye show yake lakini hatukua tumefikia muafaka, nikampa namba ya Meneja wangu wawasiliane na Meneja wake lakini hawakuwasiliana na hakuna makubaliano yoyote ya kikazi yalifanyika”
“Kitendo cha kutumia jina langu bila makubaliano yoyote kwangu nimekuchukulia ni kuchukuliana poa au kama ni dharau, mimi na Team yangu hatujapendezwa na hilo…… mimi sina tatizo kum-support Msanii yeyote ila ni lazima tuwe kwenye makubaliano kwasababu sisi wote ni Brand” —Jux.
Upande wa Harmonize haujapatikana kulizungumzia hili lakini Jux amesema alimuandikia aondoe jina lake na kumuachia comment kwenye instagram yake ikisomeka “Tafadhali hakikisha kuna makubaliano kati ya uongozi wangu na Team yako kabla ya kuniweka kwenye mabango ya matangazo kama haya”- Jux
“Tunapenda kushirikiana kama Wasanii ila taratibu za kiuongozi zifuatwe, ni vyema ukafuta hili tangazo haraka” ——— alimalizia Jux kwenye comment. #MillardAyoENT