Mwimbaji Staa wa Bongofleva Ben Pol ameiambia AMPLIFAYA ya Clouds FM kwenye Exclusive Interview kuwa hakuifurahia ndoa yake kama alivyotarajia na kukiri kuwa hali ilikua tofauti na jinsi Watu wengi kwa nje walivyokuwa waki-imagine kupitia picha mbalimbali alizokuwa akiziweka mtandaoni.
Kwa mara ya kwanza Ben Pol amefunguka kwa undani mbele ya millardayo , fridaamani na vidox kuhusu maisha yake ya ndoa na sababu kuu iliyoivunja na kusema haku-enjoy matunda ya ndoa kama alivyoziona ndoa nyingine “yani sisi sanasana naweza nikasema ilikua ni kaa hapo upige picha, paaa paa weka nini……. sisemi kwa ubaya na wala sipo hapa kwa ajili ya kumpeleka Mtu mwingine chini ila tu kwa mtazamo wangu mimi naona kama niliingia kwenye picha kuleta ule ukamilifu”