AyoTV

EXCLUSIVE: “Wazazi wangu wamenitenga kisa Wanangu walemavu, Baba anataka kunifunga, nimeleta nuksi” (+ video)

on

Isabela Gohage ( 37) ni mkazi wa mtaa wa Maramba mawili DSM mwenye Watoto sita ambapo watatu kati yao ni walemavu, Johnson hawezi kutembea anajivuta tu, Joshua hawezi hata kukaa ni Mtu wa kulala tu na hawezi hata kula analishwa , Prestigijas hawezi kukaa mwenyewe mpaka afungwe na kanga au kamba kwenye kiti chake maalum.

Mumewe alikuwa anafanya kazi ya kusaga nafaka kwenye mashine ya Mtu mmoja Kimara lakini ofisi yao imevunjwa wakati wa upanuzi wa Barabara na sasa hana kazi, wote wanaishi kwa kutegemea vibarua vya kulima, kubeba tofali nk

Isabella anadai Wazazi wake na baadhi ya Ndugu wamemtenga wakiamini amewaletea mkosi/ uchuro kwenye ukoo kwa kuzaa Watoto walemavu mfululizo kwani huko nyuma hawakuwahi kushuhudia kitu kama hicho “tangu 2014 sijawaona wala kuongea na Mama na Baba, nimetengwa”

Ukiguswa unaweza kumsaidia Isabella kupitia namba za Mdogo wake 0787454103 au 0718889485 (Lightness Maina)

MWANAMKE ALIEWAOA WANAUME WATATU “NIMEWAPA NYUMBA, NINA MIMBA, NATAKA MUME WA NNE”

Tupia Comments