Top Stories

Exclusive:Injinia kafunguka daraja la Milioni 31 “Magogo yaliyotumika hapa ni 121”

on

Baada ya kusikia huko Morogoro kwenye Kijiji cha Isago, Kata ya Mngeta, Jimbo la Mlimba Wilayani Kilombero daraja la miti limejengwa kwa MILIONI 31 wengi walihamaki na kuhisi kuna upigaji umetokea. Reporter  wako Millard Ayo  alifunga safari hadi kijijini Isago, umbali wa kilometa 305 kutoka Morogoro Mjini na kuweka kambi kwa muda kuomba kupewa hesabu ya hiyo fedha milioni 31 imetumikaje, Meneja wa TARURA Kilombero Injinia Robert Magogo na Mbunge wa Jimbo hilo Godwin Kunambi waliketi kueleza yote kupitia AYO TV na Millardayo.com

“Kulingana na Gharama ndio maana tumeanza daraja ambao hili sio la kudumu ni la mbao kama tungejenga la Chuma ama la Zege gharama ingekuwa ni kubwa  kiasi kwamba itabidi tuombe Pesa Serikali Kuu ambayo ingechukua muda sana“- Injinia Robert Magogo

“Daraja hili la Mbao kutoka hapa juu mpaka lilipoishia chini ni kama Mita 6 na kama tungejenga daraja la chuma kwa uzoefu wangu basi Gharama kukamilika ni Bilioni 1.2 na tulishafanya hivyo kwenye mto kiansi na kama la tungejenga la Zege basi lingegharimu kama Shilingi Bilioni 3”– Injinia Robert Magogo

“Mbao zilizotumika hapa ni aina ya mkarati sifa zake kwamba upo imara hata kama ukikaa kwenye maji, idadi ya magogo yaliyotumika hapa 121 ambayo yana urefu wa mita 7 kwa unene usiopungua futi moja kwasababu zinatofautiana kuna nyingine ni nene zaidi na nyingine ni nyembamba lakini haipungui zaidi ya futa mita moja , mbao ziko 245 lakini kwa size tofauti”- Injinia  Robert Magogo

Bonyeza play ufahamu ukweli wa daraja hilo lililojengwa kwa Milioni 31

RAIS AAGIZA WATAKAOCHOMWA CHANJO WALIPWE DOLA 100, WENGINE KUPIMWA

 

 

 

Tupia Comments