Top Stories

EXCLUSIVE: Mpaka nyumbani kwa Mkojani “nilienda kwa waganga, nimejulikana mwaka jana”

on

Mkojani ni muigizaji wa filamu Tanzania ambaye amejizolea umaarufu kwa siku za hivi karibuni baada yakuonekana kwenye Filamu na vichekesho ambapo amesema amekaa kwenye sanaa kwa zaidi ya miaka 17 lakini ameenza kujulikana zaidi mwaka mmoja uliopita baada yakupambana kwa muda mrefu.

Mkojani anasema kwa sasa anawasimamia wasanii 15 kutoka sehemu mbalimbali Tanzania kwa lengo lakiwasaidia lakini kabla yakujulikana alishawahi kwenda kwa waganga ili wamsaidie aweze kutoka lakini ilishindikana nakusema kilichomsaidia ni kumuamini Mungu.

“hii kujulikana nina mwaka lakini nimeanza hii sanaa miaka kumi na saba iliyopita, kuna kipindi nilienda kwa waganga ili wanisaidie lakini mwisho wa siku unakuja kugundua mganga mkubwa ni Mungu mwenyewe,namshukuru Mungu nina wasanii kumi na tano kutoka mikoa mbalimbali ambao nawafundisha vile nilivyopita na wao ndio wamekuwa wakinisaidia”-Mkojani

EXCLUSIVE: MAISHA YA DOGO SELE BUZA “NATAKA KUWA RAIS,UKIANZISHA NAMALIZA, NASOMA LA PILI”

 

 

 

 

Soma na hizi

Tupia Comments