Michezo

Simba SC yapoza machungu ya UD Songo kwa JKT Tanzania

on

Wekundu wa Msimbazi Simba SC leo imecheza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania bara dhidi ya JKT Tanzania, game ikichezwa uwanja wa Uhuru Dar es Salaam JKT Tanzania wakiwa wenyeji.

Simba SC ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo wameanza kwa kishindo kwa kufanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-1, magoli ambayo yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya 3 na 58 kabla ya Miraji Athumani kufunga goli la mwisho dakika ya 73.

Goli pekee la JKT Tanzania lilifungwa na Edward Songo dakika ya 87, baada ya mchezo huo Ligi Kuu Itasimama kupisha michezo ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2022, Tanzania itacheza na  Burundi Septemba 4 na marudiano uwanja wa Taifa Septemba 8 2019.

Soma na hizi

Tupia Comments