Kiungo zamani wa Club za Arsenal na Man City raia wa Ufaransa Samir Nasri kwa zaidi ya siku kadhaa sasa amekuwa akihusishwa kutaka kujiunga na Club ya West Ham United ya England katika dirisha dogo la usajili la mwezi January.
Nasri ambaye anatumikia kifungo cha miezi 18 bila kujihusisha na soka kwa kosa la kugundulika kutumia dawa zisizoruhusiwa michezoni, adhabu yake itamalizika December mwaka huu na amekuwa akihusishwa kurudi England kuitumikia West Ham United ikidaiwa anataka mshahra wa pound 100000 kwa wiki.
Leo November 12 2018 imeripotiwa taarifa za kuwa Nasri anakaribia kujiunga na West Ham United kwa mkataba wa miezi sita, mkataba ambao utamfanya alipwe mshahara wa pound 80000 kwa wiki na sasa anaripotiwa kukaribia kufanya vipimo vya afya, Nasri amewahi kucheza Arsenal (2008-2011), Man City (2011-2017) na baadae Sevilla kwa mkopo.
Hakuna anayemkuta Samatta kwa sasa Jupiter Pro League 2018/19