Michezo

Aussems Simba imepata point 3 lakini hajafurahishwa

on

Kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems pamoja na kikosi chake cha Simba SC kujihakikishia point 3 leo kwa kuifunga KMC kwa magoli 2-1 lakini ameeleza kuwa hajafurahishwa na namna au kiwango cha wachezaji wake walichokionesha katika mchezo huo.

“Leo hatujacheza mchezo mzuri, kiwango hakikuwa tulichokitegemea, lakini hilo linatokea kwenye mpira, hatimaye tumepata tulichokuwa tukitafuta”- Kocha Patrick Aussems baada ya mchezo wa leo dhidi ya KMC FC”>>> Patrick Aussems

Simba SC walipata ushindi dakika za lala salama kwa mkwaju wa penati baada ya mchezaji wa KMC kuushika mpira katika eneo la hatari, Simba SC sasa wanaendelea kupunguza viporo yake na wanaendelea kupanda hadi nafasi ya pili kwa kuwa na point 66 wakicheza michezo 26.

Simba na Yanga za kataa kuungana ili kucheza na Mabingwa mara 5 wa Europa League May 23

Soma na hizi

Tupia Comments