Michezo

FA waisogeza mbele EPL kwa siku 27 zaidi

on

Chama cha soka nchini England (FA) kimetangaza rasmi leo kurefusha muda wa kuruhusu mechi za soka kuendelea kuchezwa kama kawaida nchini England.

FA wametangaza kuwa michezo yote ya soka ikiwemo Ligi Kuu England itarejea tena April 30, hilo likiwa ni ongezeko la siku 27 zaidi kutoka tarehe ya awali kuwa April 3.

Hata hivyo kurefusha huko muda kurejea ama kutorejea ifikapo April 30 kutategemeana na hali ya mlipuko wa virusi vya corona kama itakuwa imerudi sawa na  endapo itakuwa imeongezeka basi yanaweza kuchukuliwa maamuzi mengine.

Soma na hizi

Tupia Comments