Habari za Mastaa

Ni Mwana FA na AY miaka 13 iliyopita kwenye hii hit yao kali kabisa mtu wangu…. (Video)

on

ay_na_fa2Ambwene Yessaya aka ‘AY‘ pamoja na Hamis Corleone Mwinjuma aka ‘Mwana FA‘ ni washkaji ambao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu sana… Walikuwa pamoja kwenye Crew ya East Coast Team na baadae wakajitoa kwa pamoja, safari yao na game ya muziki haikuishia hapo, mzigo ukaendelea kupigwa mpaka leo tunavyowaona bado wako pamoja.

Nimeamua kukurudisha nyuma mtu wangu miaka 13 iliyopita kwenye hii collabo yao ambayo walimshirikisha Banana Zoro na Ray C hii singo inaitwa ‘Safi Hiyo’, wakali wengine kama akina Crazy Gk na DJ Steve B ‘Dj Skillz’ wameonekana pia.

Kampuni iliyoshughulika na utengenezwaji wa hii video inaitwa Tripod Media na upande wa audio ilitengenezwa Backyard kwenye mikono ya Producer Abdiel Mengi…Bonge Fleva imesafiri safari ndefu mtu wangu, enjoy na hii hit ya kitambo ya wakali hao kwenye ubora wao.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments