Michezo

Fabregas asamehe mshahara wa miezi minne Monaco

on

Kiungo wa zamani wa Chelsea na Arsenal raia wa Hispania Cesc Fabregas ameripotiwa kuwa tayari kusamehe mshahara wake wa miezi minne anaolipwa na AS Monaco ya Ufaransa.

Fabregas yuko tayari kusamehe mshahara huo ambao ni pound milioni 2 (Tsh Bilioni 5.7) kwa kipindi cha miezi minne ili kuinusuru club kuyumba wakati huu wa virusi vya corona na kuomba waongezewe staff wao wa uwanja wa mazoezi ambao nao wamekatwa 30% ya mshahara.

Pamoja na hayo baada ya kufanya hivyo pia Fabregas katika mshahara wake wa pound 105000 kwa wiki (Tsh milioni 302) alikubali kukatwa asilimia 30 ili kuinusuru AS Monaco na anguko la kiuchumia lilikosababishwa na Corona.

Soma na hizi

Tupia Comments