Top Stories

Facebook, Instagram, Whatsapp zinaongoza Tanzania

on

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dr. Faustin Ndugulile amesema Tanzania ina Watumiaji wa mitandao ya kijamii milioni 16.5 ambapo Facebook na Whatsapp ndio zinaongoza kwa kuwa na Watumiaji zaidi ya milioni sita wakati Instagram ikiwa na Watumiaji milioni 4.5.

Waziri Ndugulile amesema kwa usajili wa line kwa sasa ni zaidi ya milioni 50 na Watumiaji wa internet wakiwa takribani milioni 30 na wanaofanya miamala ya fedha ni zaidi ya milioni 32.

Dkt. Ndugulile ametoa tathmini hiyo wakati wa uzinduzi wa mfumo wa kielectroniki wa uratibu na ufuatiliaji wa shughuli za kiserikali utakaosaidia kuweka uwazi na uwajibikaji na kufikisha taarifa kwa umma.

WIZARA “GWAJIMA ATHIBITISHE HUO UZOMBI, ANAHATARISHA MAISHA TUTAMSHUGHULIKIA”

Soma na hizi

Tupia Comments