Michezo

Fahamu kwanini Paundi milioni 200 zinahusika Manchester United.

on

united

 

Baada ya msimu ambao Manchester United ilimaliza kwenye nafasi ya nne kwenye ligi kuu ya England , mshambuliaji raia wa Uholanzi Robin Van Persie amethibitisha kuwa klabu hiyo imejipanga kutumia fedha zaidi ili kurudisha hadhi yake na mafanikio ambayo imepotea kwa misimu miwili mfululizo.

RVP amethibitisha kuwa United itatumia jumla ya paundi milioni 200 katika usajili wa majira ya kiangazi ikiwa ni mpango mkakati wa kurudisha heshima ya klabu hiyo ambayo imepotea tangu kocha wa zamani Sir Alex Fergusson alipostaafu .

Hii itakuwa mara ya pili kwa United kutumia kitita kama hicho cha fedha ndani ya misimu miwili baada ya kutumia kiasi hicho cha fedha kuwasajili Ander Herrera, Angel Di Maria , Luke Shaw , Daley Blind na Radamel Falcao ambaye alisajiliwa kwa mkopo ambao thamani yake ilikuwa paundi milioni 12.

Robin Van Persie amewaambia waandishi wa habari kuwa United itatumia paundi milioni 200 kusajili wachezaji wapya .

Robin Van Persie amewaambia waandishi wa habari kuwa United itatumia paundi milioni 200 kusajili wachezaji wapya .

Tayari United imemsajili kiungo mshambuliaji raia wa Uholanzi Memphis Depay toka klabu ya PSV Eindhoven na uthibitisho huu toka kwa Robin Van Persie unamaanisha kuwa wachezaji zaidi wanatarajiwa kuingia ndani ya geti la Old Trafford kabla ya kuanza kwa msimu wa mwaka 2015/2016.

Wakati hayo yakiendelea Mustakabali wa Robin Van Persie mwenyewe bado haujafahamika kwani kumekuwa na taarifa kadhaa zinazomhusisha na kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kushindwa kuonyesha kiwango bora kwa misimu miwili mfululizo .

RVP anaingia kwenye mwaka wa mwisho wa mkataba wake ndani ya Old Trafford na kuna uwezekano wa United kushindwa kupata fedha yoyote kwake endapo atamaliza mkataba wake .

Tupia Comments