Top Stories

Familia yanusurika kifo kisa mashamba

on

Familia ya mzee Manyanda Luvubu inayoishi katika kijiji cha Kibuye kata ya Bukuba wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma imenusuruka kifo mara baada ya kuvamiwa majira ya usiku wakiwa wamelala na kupatiwa kichapo kwa kutumia fimbo na mapanga lakini pia nyumba waliyokuwa wamelala kubomolewa.

Mzee Manyanda anaeleza chanzo ni ugomvi wa mashamba baina ya Aston Kipampo na Lucas Ndabo ambapo mzee Manyanda aliombwa kuwa shahidi kati yao jambo lililoanzisha mgogoro mkubwa mara baada ya kusuluhisha mgogoro huo.

Siku chache baadaye mzee huyo akiwa amelala alivamiwa na vijana na kupigwa kwa kutumia panga ambapo alipasuliwa eneo la pua na mkewe ambaye alipoteza fahamu kutokana na kipigo kikali alichopatiwa na watu hao ambapo mke wa mtoto wake mzee Manyanda aliyekuwa amefungiwa ndani wakati watu hao wakitekeleza tukio hilo.

“UMAMUITA BABY, HONEY HALAFU UNAMUUA KWA SHOKA, WIVU WA KIPUMBAVU” KAMANDA

Soma na hizi

Tupia Comments