Hali ya utekaji nyara inaendelea kuwa chachu katika vita vinavyoendelea vya Israel na Hamas huku ulimwengu ukiyataka mataifa yanayopigana kufikia muafaka.
Familia za mateka zimechanganyikiwa na kutaka majibu kutoka kwa serikali ya Benjamin Netanyahu.
Wakati huo huo, tangazo la hivi punde la kiongozi wa Hamas Ismail Haniyeh lilikuja kama miale ya matumaini aliposema siku ya Jumanne (Nov 21) kwamba vuguvugu lake la wanamgambo lilikuwa linakaribia kufikia makubaliano ya mapatano na Israel.
Taarifa iliyotumwa na ofisi yake kwa shirika la habari la AFP ilisema: “Tunakaribia kufikia makubaliano ya usitishaji vita.”
Familia za wale waliochukuliwa mateka Oktoba 7 na kundi la wanamgambo wa Hamas lilipoanzisha mashambulizi ya kushtukiza wamekuwa wakiishinikiza serikali kuchukua hatua za haraka.