Familia za wale waliochukuliwa mateka katika shambulio baya la Hamas mnamo Oktoba 7 wanakaribia Yerusalemu katika maandamano yenye lengo la kuvutia wapendwa wao.
Shirika la habari la Reuters limechukua picha hizi za waandamanaji hao leo wakiwa wamebeba mabango yenye picha za mateka.
Wanafamilia, marafiki na wafuasi wa mateka waliondoka Tel Aviv siku ya Jumanne katika maandamano ya siku tano kuelekea Jerusalem.
Walipoanza, waliitaka serikali ya Israeli “kuwarudisha nyumbani sasa”.
Israel imesema karibu mateka 240 walichukuliwa mateka na Hamas mnamo Oktoba 7.