Michezo

Mapenzi ya Games za Play Station zamfanya shabiki huyu kuchezesha mechi akiwa jukwaani !!!!

on

Mchezo wa soka ni mchezo ambao hupendwa na watu wengi ila kitu ambacho huvutia zaidi uwanjani ni pale kila shabiki wa timu fulani anavyo furahia kwa style yake, hii ni mpya mtu wangu kwa shabiki huyu wa soka kwani amefanya kitu ambacho kinafurahisha na kustaajabisha.

Ed Syers ambaye anafanya kazi katika kampuni ya takwimu alikuwa mmoja kati ya mashabiki wa soka walio hudhuria mechi ya Newcastle Unieted dhidi ya Arsenal katika uwanja wa St James ParkEd Syers aliingia uwanjani na kifaa cha kuchezea Games wakati mechi ikiendelea na yeye alikuwa na mzuka wa kubonyeza mashine yake yaani kama yeye ndio anachezesha mechi katika Play Station.

CNkwnDKWgAAXKcT

Richard Mason ambaye alikuwa mmoja kati ya watu waliokuwa wamekaa karibu ya Ed Syers alimpiga picha na kuiweka katika mtandao wa twitter, hivyo kufanya watu kuanza kustaajabu, Ed Syers anaonekana kuwa mpenzi wa Games za Play Station. Hata hivyo mechi ilimalizika kwa Arsenal kushinda goli 1-0.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia za siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>Videos

Tupia Comments