Michezo

Liverpool yazidi kupunguzwa kasi, mashabiki nao walisusia mauzo ya tiketi!!

on

liverUkizungumza ushabiki klabu ya Liverpool huenda ndio inayoongoza kwa kuwa na mashabiki wanaopenda zaidi timu yao na kutoa sapoti ya kutosha pale timu inapocheza hata ikitokea imefungwa.

Lakini kitendo cha mauzo ya tiketi kupanda ghafla na kufikia pauni 48 wakati timu yao ilipokuwa ikicheza na Hull City jana kiliwaudhi mashabiki hao na kususia mchezo wao dhidi ya Hull City ambao walijikuta wakifungwa bao 1-0.

faaa

Matokeo hayo yameifanya Liverpool kupoteza malengo yake ya kuwa kwenye timu tano za juu kwenye msimamo wa ligi kuu ya England baada ya jana kukubali kichapo hicho.

fans

Mashabiki hao waliandamana kupinga kiasi kikubwa ambacho wamekuwa wakilipa kama tiketi za kuingia uwanjani na kuomba bei hiyo ipunguzwe ili waweze kushuhudia timu yao kila inapocheza.

fans3

Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia Twitter, Instagram na Facebook ukijiunga na mimi kwa kubonyeza>>>twitter Insta Facebook

Tupia Comments