Wasafiri wote wanpenda usafiri wa haraka, salama na wa uhakika.. sasa inapokuja kwenye teknolojia wenzetu wametuacha mbali kiukweli.. Kwa TZ ukitaka kusafiri haraka kwenda zako Mwanza au Mbeya inabidi tu upande zako Fast Jet ili uwahi.
Niliwahi kukuletea story toka Spain, mtu anakaa umbali kama wa Dar-Moro, anaishi Morogoro anafanya kazi Dar.. na kila siku anawahi kazini, usafiri unaotegemewa zaidi ni treni za umeme. Japan wanaingia kwenye HEADLINES za maendeleo mengine kwenye Teknolojia, wametengeneza treni ambayo inasafiri umbali wa Kilometa 603 kwa saa moja.. hesabu ya kwanza nikawaza kama ni safari ya Mbeya inachukua saa 1 na nusu, kwa sababu Dar-Mbeya ni Kilometa kama 840 hivi.
Mwanza je? Dar-Mwanza ni kama kilometa 1,150.. hiyo safari inakamilika ndani ya saa mbili tu !!
Japan wana mpango wa treni hiyo kuanza kazi kati ya miji ya Tokyo na Nagoya mwaka 2027, Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe atakuwa Marekani ndani ya wiki hii kuangalia jinsi watakavyoweza kujenga reli kwa ajili ya treni hiyo kati ya New York na Washington D.C.
Kingine cha kukufikishia ni kwamba tumezoea kuona treni zenye tyre za chuma ambazo zinatembea kwenye reli, hii inatumia sumaku ambazo zinatumia umeme.
Unaweza kuiangalia kwenye video hapa treni hiyo ikiwa kwenye majaribio..
https://www.youtube.com/watch?v=FNleI1eHzi0
Unahitaji chochote ninachokipata kisikupite? jiunge na mimi kwenye Twitter, Facebook na Instagram kwa kubonyeza hapa >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa>>>>Videos ili kila video ya AyoTV ikufikie.