Michezo

FAZ yampiga chini Kalusha Bwalya

on

Legend wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia Kalusha Bwalya, jina lake limeondolewa katika kinyang’anyiro cha kugombea Urais wa chama cha soka Zambia (FAZ).

Uchaguzi mkuu wa FAZ utafanyika March 7 2020 na inadaiwa kuwa Kalusha kaondolewa kwa kushindwa kukidhi vigezo vya kimaadili na jina lake likaafikiwa kukatwa.

Mchezaji huyo bora wa Afrika wa mwaka 1988 anaondolewa katika mbio hizo na kuwaacha Andrew Kamanga, Joseph Nkole na Emmanuel Munaile majina yao kupitishwa, wengine walioshindwa ni Ricky Manfunda, Suzyo Zimba na Richard Kazala ila wana nafasi ya kukata rufaa kabla ya February 17 2020.

Soma na hizi

Tupia Comments