Kila siku asubuhi huwa nazisogeza headlines zilizobebwa kwenye kurasa za Magazeti ya Tanzania, Uchambuzi wa stori zote napandisha kwenye account yangu ya Twitter >>>@millardayo. Tayari nimezikusanya na waweza kuzipitia hapa chini moja baada ya nyingine.
Moja ya yaliyondikwa kwenye gazeti la Nipashe ni ripoti ya utafiti huu wenye kichwa cha habari ‘Chips dume zinavyoweza kuwa chanzo cha sukari’
#NIPASHE UTAFITI:Mihogo ya kukaanga ni miongoni mwa vyakula vilivyobainika kuwa chanzo cha kisukari 'type2 diabetes' pic.twitter.com/2lA0TO572p
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
Gazeti la Nipshe limeripoti kuwa pengine hii ni taarifa ya kushtua kuhusiana na masuala ya afya, hasa kwa wakazi wa mijini. Ni kwamba mihogo ya kukaanga maarufu kama ‘chips dume’ ni miongoni mwa vyakula vilivyobainika kuwa vinaweza kuwa chanzo cha aina mojawapo ya maradhi ya kisukri (type 2 diabetes).
Aidha, mbali na chips dume, vyakula vingine vyote vinavyokaangwa kwa mafuta vinaweza kuwa chanzo cha maradhi hayo ya kisukari endapo uandaaji wake hautafanyika kwa kuzingatia tahadhari za kiafya.
Kwa mujibu wa ripoti ya utafiti iliyotolewa hivi karibuni, ni kwamba vyakula vilivyoandaliwa kwa kuchemshwa au kuivishwa kwa mvuke ndiyo pekee vilivyo salama zaidi kwa sababu ya kutokuwa na tishio hilo la kisukari kwa walaji, wakati mihogo, viazi na vyakula vingine vinapokaangwa au kuokwa au kuchomwa hutoa kemikali iitwayo glycation.
Aidha, kunapokuwa na kiwango cha juu cha kemikali hiyo, matokeo yake huwa kunatokea ukinzani dhidi ya insulin kwa mlaji wa chakula husika na matokeo yake ni uwezekano wa maradhi ya kisukari kwa mujibu wa ripoti ya utafiti huo.
Kwa kawaida insulin ni aina ya kichocheo (homoni) ndani ya mwili ambacho husaidia kurekebisha kiwango cha sukari ambacho ni chanzo cha nishati mwilini. Bila ya kuwa na insulin au kukiwa na ukinzani dhidi ya insulini, kiwango kikubwa cha sukari hubaki kwenye damu. Hali hiyo pia inaweza kusababisha matatizo ya moyo, macho, figo, na ogani nyingine mwilini.
Unaweza kupitia habri nyingine zilizoandikwa kwenye magazeti ya Tanzania September 18 2016
#NIPASHE Prof. Lipumba ahusishwa na kula njama za kutaka kuiangamiza CUF pia ahusishwa na fedha za michango mil 280 pic.twitter.com/udOH7kWrVp
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#NIPASHE Baadhi ya wadau watilia shaka uamuzi wa TCU kupunguza alama za ufaulu, wadai unahatarisha ubora wa elimu pic.twitter.com/vDL6lDPQIc
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#NIPASHE Raia wa Oman anayedaiwa kufanya vurugu na kuchelewesha ndege kuondoka JNIA aendelea kusota polisi pic.twitter.com/19hFrnUxqX
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#NIPASHE Baraza la madiwani K'ndoni limevunjwa rasmi kufuatia serikali kuigawa halmashauri ya manispaa hiyo kuwa 2 pic.twitter.com/rvVTjM07q7
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#MWANANCHI Nyumba 21 zimebomoka baada ya mvua ya mawe iliyoambatana na upepo mkali kunyesha Mtimbwa, Sumbawanga pic.twitter.com/Uh6hbcbxDk
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#MWANANCHI Serikali yaagiza wizara kuanzisha mifumo ya kielektroniki ktk utunzaji badala ya kuhamia Dom na mafaili pic.twitter.com/gvyxjJo0Nq
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#MWANANCHI CDA yatafuta mwekezaji kuboresha ukumbi wa zamani wa disko wa NK Dodoma ili utumiwe na wizara au idara pic.twitter.com/BSa1XQkwHO
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
#JamboLEO JPM asema serikali itarekebisha miundombinu iliyoharibika Kagera na waliobomokewa nyumba wazirekebishe pic.twitter.com/mXzQuiHTi8
— millardayo (@millardayo) September 18, 2016
ULIKOSA HII YA RAIS MAGUFULI KUPOKEA MSAADA KUTOKA KENYA NA UGANDA KWA JILI YA MAAFA YA KAGERA? UNAWEZA KUIANGALIA VIDEO HII HAPA CHINI