Michezo

FC Barcelona waitumia Corona kama fursa kuuza Barakoa

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania imetumia ugonjwa wa Corona kama fursa ya kuingizia club yao mapato kwa kutengeneza face masks (Barakoa) zenye nembo ya club.

Barakoa hizo zilizotengenezwa kwa material ya pamba kwa asilimia 100 zitapatikana katika maduka ya FC Barcelona kwa kiasi cha pound 16 ambazo ni zaidi ya Tsh elfu 45.

Inaripotiwa kuwa kutakuwa na aina zaidi ya 9 za Mask hizo zinazozalishwa na Barcelona, Ligi Kuu ya Hispania 2019/20 inatajwa kuwa itarejea June 12 yaani siku 4 baadae baada ya serikali kuruhusu michezo na Ligi kurejea.

Soma na hizi

Tupia Comments