Michezo

FC Barcelona yasajili nje ya dirisha la usajili LaLiga wakitoa baraka

on

Club ya FC Barcelona ya Hispania imethibitisha kumsajili mshambuliai wa timu ya taifa ya Denmark Martin Braithwaite kutokea Leganes kwa mkataba wa miaka minne, Barcelona wandaiwa kutia nguvu zaidi katika kuboresha safu yake ya ushambuliaji baada ya kuumia kwa Ousmane Dembele.

Mkataba wa Martin Braithwaite ndani ya FC Barcelona utamalizika June 2024,dau la euro milioni 18 ambayo ni zaidi ya Tsh bilioni 44.8 ndio limemtoa Martin Braithwaite katika club ya Leganes na kujiunga Nou Camp.

Martin Braithwaite anaungana na kikosi cha FC Barcelona wakati huu ikiwa ni nje ya dirisha la usajili kwa sababu Barcelona wametumia sheria ya LaLiga kusajili mchezaji aliye nje ya dirisha la usajili kama mchezaji wao wa nafasi hiyo ameumia na kuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya miezi mitano kama ilivyo kwa Dembele aliye nje ya uwanja kwa miezi sita.

VIDEO: MECKY AGOMA KUMTUPIA ZIGO LA LAWAMA TINOCO KIPIGO CHA 1-0 CHA SIMBA

Soma na hizi

Tupia Comments