Michezo

FC Bayern Munich ya Hansi Flick bado ya moto UEFA

on

Club ya FC Bayern Munich imeendelea kuwa na wakati mzuri katika michuano ya UEFA Champions League baada ya kupata ushindi wa magoli 4-0 dhidi ya Atletico Madrid.

Magoli ya FC Bayern Munich yamefungwa na Kingsley Coman dakika ya 28 na 72, Groetzka dakika ya 41 na Tolisso dakika ya 66 na kuifanya Bayern kuvuna point tatu zao za kwanza za Kundi A msimu wa UEFA 2020/21.

Hata hivyo FC Bayern Munich chini ya kocha wao Hansi Flick wanaendelea kuwa na wakati mzuri zaidi, hii ikiwa ni game yao ya 9 mfululizo ya UEFA Champions League chini ya kocha huyo wakiwa wameshinda game zote ma kufunga jumla ya magoli 34 na kufungwa magoli manne pekee.

Soma na hizi

Tupia Comments