Michezo

FC Porto kumuacha Mbemba kisa kudanganya umri

on

Club ya FC Porto ya Ureno kuna uwezekano ikaachana na beki wake Chancel Mbemba raia wa Congo DR baada ya kugundua kuwa mchezaji huyo amedanganya umri wake, Mbemba inaelezwa kuwa ana tarehe 4 tofauti za kuzaliwa zilizopo katika vyeti vyake vya kuzaliwa vinnen tofauti tofauti.

Mbemba ambaye kwa sasa anadai kuwa na umri wa miaka 27 inatajwa kuwa anaweza kuwa mkubwa kwa miaka mitano zaidi 32, Porto wanataka kumuacha mwisho wa msimu AC Milan na vilabu kadhaa Ulaya vilikuwa vikimuhitaji lakini tuhuma za kudanganya umri zimefanya wasite.

Mbemba inadaiwa kuwa alidanganya umri 2012 wakati anaondoka Congo DR na kwenda kuanza kucheza soka la kulipwa katika club ya Anderlecht ya Ubelgiji.

Soma na hizi

Tupia Comments