Tume ya ushindani FCC imekubaliana na jumuiya ya wafanya biashara wa soka kuu la kimataifa kariakoo kufanya msako na ukaguzi wa pamoja wa bidhaa bandia kutokana na uwepo wa ongezeko la bidhaa bandia katika soko hilo na kusababisha hasara kwa wauza bidhaa halali na wanaonunua bandia kutokupata thamani halisi ya fedha zao.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na mkurugenzi wa FCC Bw. William Erio wakati amekutana na uongozi wa jumiya ya wafanya biashara wa kariakoo kwenye ofisi za tume ya ushundani.
“Wafanye biashara halali kwa manufaa yao wenyewe ,wasije tumia fursa ya wafanyabishara halali wakitizama wakaona wananufaika nao wanapenyeza biashara bandia katika bidhaa zinazofanana na zile ambazo ni halali”.
Akizungumza Kwa niaba ya jumiya ya wafanya biashara wa kariakoo Bw.Martine Mbwana ambae ni mwenyekiti wa jumuia hiyo amesema
“Naomba kuwatoa wasiwasi wafanya biashara wote wa kariakoo kuwa tume ya ushindani FCC tumekubaliana kwa pamoja kushirikiana kwenye zoezi hilo la kukamata na kutokomeza Kabisa bidhaa bandia kwenye soko la kariakoo”.