Michezo

FCC wamkana MO Dewji “hatujakwamisha mabadilko Simba”

on

Tume ya ushindani (FCC) imetoa maelekezo kuwa haijakwamisha mchakato wa mabadiliko wa Simba SC kama ilivyoripotiwa na muwekezaji wao MO Dewji.

FCC ilisitisha kwa muda mchakato wa mabadiliko kwa sababu mbalimbali ikiwemo kutaka ufafanuzi kutoka Simba SC ni utaratibu gani wametumia kumpata CEO wa club October 13 2020.

Kama utakumbuka vizuri hivi karibuni katika mkutano wa MO Dewji na waandishiwa habari alinukuliwa akisema kuwa amekuwa mvumilivu kuhusu suala la mchakato wa mabadiliko na wao kama Simba SC wamekamilisha kila kitu ila FCC ndio bado hawajakamilisha.

Soma na hizi

Tupia Comments