Top Stories

Mmiliki wa Facebook amjibu Trump kuhusu ‘tuhuma’

on

Mmiliki wa mtandao wa Facebook Mark Zuckerburg amkanusha madai ya Rais Trump wa Marekani kuwa kampuni hiyo iko kinyume naye na kumpinga.

Jana September 27, 2017 Trump aliandika kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa mtandao huo wa Facebook umekua kinyume naye hasa katika kampeni za uchaguzi mkuu wa nchi hiyo mwaka 2016 huku Zuckerberg akieleza kuwa pande zote mbili za kisiasa wakati wa kampeni hizo hazikufurahishwa na maoni yanayotolewa na watumiaji wa mtandao huo.

Facebook, Twitter na Google zimeombwa kutoa ushahidi mbele ya kamati ya kijasusi ya bunge la seneti Marekani Novemba 1 kuhusu tuhuma za Urusi kuingilia uchaguzi huo na hivi karibuni Facebook itawasilisha matangazo ya kisiasa 3,000 kwa wachunguzi wa serikali wanaochunguza tuhuma hizo.

Ulipitwa na hii? “Ninao ushahidi Madiwani wanaohamia CCM wananunuliwa” – MBUNGE NASSARI

 

Soma na hizi

Tupia Comments