Top Stories

NAPE NNAUYE! Kamwandikia Tundu Lissu saa 19 baada ya kushambuliwa

on

Moja ya habari iliyoshtua watu wengi September 7, 2017 ni tukio la kushambuliwa kwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambapo watu wasiojulikana walimpiga risasi akiwa kwenye gari nyumbani kwake wakati anatokea Bungeni.

Kutokana na tukio hilo watu wengi wamekuwa wakilielezea kwa hisia tofauti na miongoni mwa watu hao ni pamoja na wanasiasa, viongozi wa dini, serikali na mastaa wa muziki.

Mmoja wa wanasiasa waliolizungumzia tukio hilo ni Mbunge wa Mtama, Nape Nauye ambaye aliandika kwenye Twitter yake akielezea kuwa pamoja na Mbunge Lissu saa chache kabla ya kushambuliwa.

Nape kaandika>>>”Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa the T460CQV uliyoilalamikia!”

BREAKING NEWS: TAMKO LA CHADEMA KUHUSU KUSHAMBULIWA KWA RISASI TUNDU LISSU!!!

Soma na hizi

Tupia Comments