Top Stories

Watafiti wamejibu kwa nini mtu huchelewa kulala au kutopata usingizi ugenini

on

Inawezekana wewe ni mmoja kati wa watu ambao hukosa usingizi kabisa au kushindwa kulala vizuri pindi unapotembelea sehemu tofauti na uliyoizoea kama vile ugenini, hotelini na sehemu nyingine na unajiuliza ni kwa sababu ipi inakufanya uchelewe kulala au kutolala kabisa.

Sasa leo September 3, 2017 nimekusogezea hii stori ambapo unaambiwa Wanasayansi wameelezea kuhusu kwa nini mtu hukosa usingizi au kutolala vizuri akiwa ugenini wakisema husababishwa na ubongo.

Mtu anapolala ugenini au mahala asipopazoea nusu ya ubongo wake ndiyo hulala lakini nusu nyingine inakuwa ‘active’ na hii ni kutokana na mabadiliko ya mazingira.

Unaambiwa jambo hili hupelekea mtu kuchelewa kupata usingizi na huwahi kuamka pengine isivyo kawaida na wakati mwingine awapo katikati ya usingizi huweza kushtuka anaposikia milio ya vitu kama ndege, mtu anatembea na vingine vingi.

HUZUNI HARUSINI!!! Mabwana harusi waugua baada ya kula chakula chenye sumu

Uliiona hii? Lissu, LHRC waungana kupinga kulipuliwa Ofisi ya Mawakili

EXCLUSIVE: AyoTV yamtembelea Mstaafu Kikwete “nanenepa siku hizi, mlikua mnanifuja” FULL VIDEO ITAZAME KWA KUBONYEZA PLAY HAPA CHINI

Soma na hizi

Tupia Comments