Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo January 12, 2018 imetoa agizo kwa shule zote ambazo ziliwarudisha nyuma wanafunzi madarasa, au kuwahamisha au kuwafukuza shule wanafunzi kwasababu hawakufikia wastani wa ufaulu husika kuhakikisha wamewarudisha wanafunzi hao shule ifikapo January 20, 2018.
Agizo hilo limeelekeza kuwa kwa shule ambayo itakaidi agizo hili, itafutiwa usajili wake pamoja na usajili wa wanafunzi wake na kuwaagiza pia wazazi wa wanafunzi hao kuhakikisha watoto wao wanarudi shule siku hiyo iliyoelekezwa.
Wizara imeeleza kuwa waraka wa elimu namba 7 wa mwaka 2004 umepiga marufuku utaratibu huo wa shule kukaririsha, kuhamisha au kuwafukuza shule wanafunzi kwa kutofaulu inavyotakiwa na kueleza kuwa kuna shule zisizo za serikali zimekuwa zikifanya makosa hayo.
“Tsh Bilioni 23 zinatolewa kila mwezi na serikali kwaajili ya elimu bure” – Ole Nasha
Waziri Kigwangalla amezindua kamati ya kuandaa mwezi wa maadhimisho ya urithi wa TZ