Mbunge wa Kibamba John Mnyika leo July 28, 2017 ameielezea hatua ya Spika Ndugai kubariki kufutiwa uanachama Wabunge wa Viti Maalumu wa CUF akisema ni makosa kwa kuwa kuna kesi Mahakamani kuhusu utata wa uongozi wa Chama hicho.
Aidha, Mnyika amemuomba Spika kutangaza wateule ambao wametangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi July 27, 2017 kuwa hawataapishwa mpaka mashauri yao yaliyopo Mahakamani yamalizike.
Hatua ya John Mnyika imekuja siku chache baada ya Spika kuridhia kufutiwa uanachama Wabunge wanane wa CUF baada ya kupokea barua kutoka kwa Mwenyekiti wake Prof. Lipumba kisha kutangaza nafasi zao kuwa wazi na kumuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi kufanya taratibu zilizostahili ambapo alitangaza majina ya Wabunge wengine wanane kuziba nafasi zao.
ULIPITWA? Prof. Lipumba baada ya Spika kuridhia Wabunge 8 kuvuliwa uanachama CUF…bonyeza PLAY kutazama kwenye VIDEO hii!!!
ULIPITWA? CUF ya Prof. Lipumba vs Maalim Seif walivyokutana Mahakamani…PLAY kwenye video hii kutazama kila kitu!!