Top Stories

INASIKITISHA: Wazazi wampiga, wanyonga na kuuchoma moto mwili wa binti yao…..kisa?

on

Mtoto wa miaka 13 ajulikanaye kwa jina la Radhika Narasimba ameuawa kikatili India baada ya kupigwa, kunyongwa na baadaye mwili wake kuchomwa moto na baba yake mzazi kutokana na kukutwa na mzazi wake huyo nje ya shule aliyokua anasoma akiwa anaongea na mvulana.

Narasimba ambaye tayari amekwisha kamatwa na polisi na kukiri kufanya tukio hilo ameeleza kuwa mtoto huyo alikua anahatarisha heshima na jina la familia yake kwa kusimama na mvulana huyo na upelelezi unaonesha kuwa mama mzazi wa mtoto huyo alihusika pia kwenye kifo cha mtoto huyo kwa kumwagia mafuta na kisha baba kuwasha moto.

Radhika ameelezewa kuwa mtoto mwenye uwezo darasani na mcheshi na marafiki aliokuwa akisoma nao wameeleza masikitiko yao juu ya kilichomkuta mwenzao huku wakilaani wazazi hao kwa ukatili walioufanya.

Ulipitwa na hii?BREAKING NEWS: Nyumba ya Zitto Kabwe ilivyoteketea (+video)

Hii je? Siku 15 tangu kukamatwa Almasi Airport, watuhumiwa Mahakamani

Soma na hizi