Michezo

Sahau kuhusu EPL, Man United wanaendelea vizuri Europa League

on

Man United usiku wa November 7 2019 walicheza mchezo wao wa UEFA Europa League dhidi ya Partizan Belgrade, game hiyo ya mtoano iliyochezwa katika uwanja wa Old Trafford mambo yamekuwa mazuri kwa Man United.

Game hiyo ya mtoano Man United ilifanikiwa kupata ushindi wa magoli 3-0, magoli ya Man United yakifungwa na Mason Greenwood dakika ya 21, Anthony Martial dakika ya 33 na Marcus Rashford dakika ya 49.

Ushindi huo umekuja ikiwa Man United imetoka kupoteza mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Bournemouth November 2, Partizan wanaonekana kutokuwa vizuri kutokana na game zao 5 zilizopita za michuano mbalimbali kufungwa tatu  na kushinda mbili.

VIDEO: BAADA YA KUFUKUZWA AYO TV IMEMFUATA ZAHERA KWAKE “SIJAPEWA BARUA”

 

Soma na hizi

Tupia Comments