Taarifa ya mwezi ya Maendeleo ya Uchumi inayotolewa kila mwezi na Benki Kuu ya Tanzania yameonesha sehemu kubwa ya fedha zinazokopwa nje hutumika kwa Usafiri na Mawasiliano.
27.2% ya deni ilitumika kwa usafiri Oktoba 2020, kwa Septemba 2021 na Oktoba 23.2% ilitumika kwa usafiri na mawalisiliano. Aidha sehemu inayofuata baada ya usafiri ni ustawi wa jamii na elimu ambayo kwa Oktoba 2021 imetumia 16.2%
Sekta ya utalii inawekewa kiwango kidogo zaidi cha fedha zinazokopwa nje ambapo kwa Oktoba 2021 ni 1.0% ya deni la nje ilitumika kwa sekta hiyo.