Michezo

Ninayo kauli ya Sir Alex Ferguson kuhusu Paul Pogba kuondoka Man United 2012

on

Kocha wa zamani wa klabu ya Manchester United Sir Alex Ferguson ambaye alistaafu kuifundisha Man United baada ya kuitumikia kwa miaka 27. Ferguson alistaafu 2013 kukinoa kikosi hicho na kuendelea kusimamia miradi yake binafsi, Ferguson ameeleza sababu za Paul Pogba kuondoka Man United na kutokubali kusaini mkataba mpya.

Ferguson aliwahi kulaumiwa kwa kushindwa kumshawishi Paul Pogba abaki Man United na wengi walifikiri hakuwa katika mipango yake hivyo ndio maana alimuacha kama mchezaji huru ajiunge na Juventus 2012.  Stori hii inakuja baada ya Ferguson kueleza kwa kina nini kilipelekea hadi Paul Pogba akaondoka klabu hiyo.

pogba

Stori ni kuwa Ferguson licha ya kutozijibu lawama zake za mwanzo kuhusu Pogba wakati ule, katika kitabu chake ameeleza kuwa moja kati ya watu waliyosababisha Paul Pogba aondoke Man United ni Mino Raiola ambaye ni wakala wa Paul Pogba.

“Kulikuwa na mawakala wawili au mmoja kiukweli simpendi Mino Raiola ambaye ni wakala wa Paul Pogba ndio alivunja mahusiano mazuri kati ya Pogba na klabu. Tulikuwa na mkataba wa miaka mitatu na Pogba na mkataba wake ulikuwa na kipengele cha kuongeza mkataba mpya ila Raiola alivuruga mipango na Pogba kujiunga na Juventus”>>> Ferguson

si

Sir Alex Ferguson

Paul Pogba alihama Man United na kujiunga na klabu ya Juventus 2012 baada ya kukasirishwa na kitendo cha kutopata nafasi ya kucheza kikosi cha kwanza cha Man United mara kwa mara. Kwa sasa Paul Pogba anayewindwa na vilabu vya Man City, FC Barcelona, Real Madrid na Chelsea anatajwa kufikia thamani ya pound milioni 70.

PAPO KWA PAPO zipate habari zote zinazonifikia kuanzia kwenye siasa muziki, michezo, maisha, Breaking news na nyingine kwa kujiunga hapa na mimi >>> Twitter Insta FB na nitakua nikikutumia kila ninachokipata pia usisahau kusubscribe YouTube kwa kubonyeza hapa >>>YouTUBE

Tupia Comments