Michezo

Fernandes kuiongoza Man United dhidi ya PSG leo

on

Kocha wa Man United Oleg Gunnar Solskjaer ametangaza kuwa nahodha wa Man United Harry Maguire hajasafiri na timu kuelekea Ufaransa katika mchezo wao wa kwanza wa Kundi H Wa UEFA Champions League dhidi ya PSG.

Solskjaer amesema kuwa katika mchezo baada ya kukosekana Maguire sasa Bruno Fernandes ndio atatumika kama nahodha wa mchezo huo, hata hivyo Man United inawakosa wachezaji kama Mason Greenwood, Eric Bailly, Jesse Lingard na Edinson Cavani.

”Najua kuwa wachezaji wote hao sio muda mrefu watarejea kikosini, Edinson anahitaji siku kadhaa za mazoezi labda tunaweza kuangalia uwezekano wa kumtumia weekend, natumai Harry (Maguire) na Greenwood wanaweza kurejea pia japo sina uhakika”>>> Solskjaer

 

Soma na hizi

Tupia Comments