Michezo

Afrika Kusini waandika historia fainali ya Kombe la Dunia Rugby

on

Timu ya Rugby ya Afrika Kusini leo imeandika historia mpya kufuatia kutwaa Ubingwa wa Rugby kwa kuifunga England kwa magoli 32-12, Afrika Kusini wametwaa Ubingwa wa dunia ambao umewafanya kuwa wametwaa kwa mara ya tatu katika historia.

Afrika Kusini Ubingwa huo waliotwaa kwa mara ya kwanza baada ya miaka 12 toka wafanye hivyo mara ya mwisho 2007, wanaweka rekodi ya kutwaa Ubingwa huo wakiwa na nahodha wa kwanza mweusi Siya Kolisi katika historia ya timu yao ya Rugby.

Sasa Afrika Kusini na New Zeland wametwaa Ubingwa huo mara tatu tatu, Afrika Kusini wakitwaa (1995, 2007, 2019), sasa Afrika Kusini unaweza kusema wanashinda Kombe hilo kila baada ya miaka 12.

VIDEO: Mpoki alivyomvunja mbavu Rais Mstaafu Kikwete

Soma na hizi

Tupia Comments