AyoTV

“Wampeleke Mahakamani, tutakutana huko” – Kibatala baada ya Lissu kukamatwa

on

Leo July 20 Mwanasheria, Mbunge wa CHADEMA na Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika TLS, Tundu Lissu amekamatwa akiwa Airport Dar es Salaam akielekea Rwanda kwenye mkutano wa Chama cha Mawakili wa Afrika Mashariki.

Ayo TV na millardayo.com zimempata Wakili wake Peter Kibatala na amezungumzia tukio hilo>>>”Mimi sijaongea naye moja kwa moja kwa sababu simu zake ni ama zimezimika au zimezimwa lakini taarifa nilizopata kutoka kwa watu wake wakiwemo ambao wamemuacha Airport muda si mrefu na wengine ninaowaamini ni yes amekamatwa na anapelekwa Central Police Station.

“Kuna Wakili mwenzangu anaelekea huko kwenda kushughulikia Haki zake za kisheria na pengine kusisitiza kwamba apelekwe Mahakamani na sisi kama ni kweli amekamatwa rai yetu ni hiyo kama wamemkamata na waliomkamata wanaamini kwamba wana tuhuma dhidi yake wakamilishe taratibu zao mapema kama inavyowezekana wampeleke Mahakamani tukakutane naye huko.” – Peter Kibatala.

FULL VIDEO: Lissu alivyogoma kutoka Mahakamani ili asikamatwe na Polisi Dodoma!!!

VIDEO: “Utaratibu unafanywa kumpeleka Edward Lowassa Mahakamani” – Tundu Lissu, mtazame kwenye hii video hapa chini akiongea yote!!!

Soma na hizi

Tupia Comments