Top Stories

MAAJABU! Panya wamshambulia mtoto wa miaka 14 hadi kulazwa hospitali

on

Unaambiwa hii imetokea Ufaransa ambapo katika hali ya kushangaza mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 14 aitwaye Samantha amelazwa hospitalini akipatiwa matibabu baada ya kuvamiwa na panya ambao walimng’ata mwili mzima na kumsababishia majeraha mengi.

Familia ya mtoto huyo imeeleza kuwa usiku wa tukio hilo walienda kulala kama kawaida lakini asubuhi walimkuta mtoto huyo anavuja damu nyingi akiwa kitandani kwake baada ya kung’atwa na panya usiku.

Baba wa mtoto, Jerome ameeleza binti yake ana ulemavu ndio sababu ya kutoomba msaada kwa familia wakati anatafunwa na panya akisema pia amemkuta binti huyo akiwa na majeraha 45 usoni, 150 mikononi na 30 miguuni.

Uliiona hii? Hekaheka ya aliyedaiwa kubaka watoto watatu, kadaiwa kubaka tena

Hii je? IDRISS KAFUNGUKA!! Ni kuhusu Wanaume wanaolelewa na wanawake

Soma na hizi

Tupia Comments