Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Neymar ameshindwa kufanya mazoezi na wenzake

on

Staa wa timu ya taifa ya Brazil anayeichezea Club ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Neymar ameripotiwa kushindwa kufanya mazoezi na wenzake wakiwa nchini Urusi baada ya kupata majeraha wakati wa mazoezi.

Neymar ameripotiwa kupata maumivu ya enka akiwa anafanya mazoezi na wenzake na kutoka nje ya uwanja kabla ya mazoezi kumalizika, baada ya kupata majeraha hayo doctor wa timu ya taifa ya Brazil Rodrigo Lasmar  ametoa taarifa rasmi ya staa huyo.

Hata hivyo Brazil pia ambao wametoka sare ya 1-1 katika mchezo wao wa kwanza dhidi Switzerland, Neymar ndio alikuwa mchezaji aliyofanyiwa madhambi mara nyingi zaidi (10) katika Kombe la Dunia toka 1998 alivyofanyiwa Alan Sheerer.

“Neymar amemuona doctor tayari na atakuwa hapa kwa leo na kesho asubuhi lakini kesho mchana ataungana na wenzake mazoezini”Rodrigo Lasmar 

FULL VIDEO: Zilivyotolewa tuzo za MO Simba Awards 2018

Soma na hizi

Tupia Comments