Michezo

VIDEO: JKT Tanzania FC Full kujikoki, timu imekabidhiwa kwa Meja Bwai

on

Club ya JKT Tanzania baada ya kuanza vizuri katika msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2019/2020 kwa kuvuna point 6 kwa kuzifunga timu za Biashara United na Kagera Sugar za Kanda ya ziwa, imerejea Dar es Salaam na kutambulisha uongozi wake mpya ambao umechaguliwa.

JKT Tanzania katika makao makuu ya club yao Mlalakuwa wamemtambulisha mwenyekiti wao mpya sambamba na kumuanga aliyekuwa mwenyekiti wao zamani ambaye ameondoka akiiacha katika mafanikio sambamba na kuacha club ikiwa na uwanja wake.

Mwenyekiti mpya wa JKT Tanzania ni Meja Javan Bwai aliyerithi kiti hicho kutoka kwa mwenyekiti aliyemaliza muda wake Hassan Mabena, sherehe ya makabidhiano imefanyika mbele ya kaimu mkuu JKT Kanali Rajab Mabele.

VIDEO: Salim Kikeke kafunguka makubaliano yake na MO Dewji ubalozi wa Simba SC

Soma na hizi

Tupia Comments