Premier Bet
TMDA Ad

Michezo

Giroud ameanza kazi tayari akiwa Chelsea

on

Tukiwa tunasubiria game ya UEFA Champions League kati ya Barcelona dhidi ya Chelsea, usiku wa February 16 Chelsea imecheza game yake ya FA Cup dhidi ya Hull City katika uwanja wao wa Stamford Bridge.

Chelsea licha ya kuwa imekuwa haifanyi vizuri katika Ligi Kuu kwa baadhi ya mechi zao kiasi cha kuhesabiwa kuwa msimu huu watashindwa kutetea taji lao, leo kwenye FA dhidi ya Hull City wamefanikiwa kupata ushindi wa magoli 4-0.

Magoli ya Chelsea yakifungwa na Willian aliyefunga magoli mawili dakika ya 2 na 32, Pedro Rodriguez dakika ya 27 na Oliver Giroud akifunga goli lake nne kwa Chelsea huku likiwa ni goli lake la kwanza toka ajiunge na Chelsea akitokea Arsenal.

Haji Manara amewasikia wanaoibeza Simba kutoka sare ya 2-2 vs Mwadui FC

Soma na hizi

Tupia Comments