Wanasayansi nchini Marekani wamebainisha kuwa tatizo la upweke linakua kwa kasi kubwa sana duniani ambapo kwa nchi hiyo takribani watu milioni 42.6 wenye umri zaidi ya miaka 45 wanateseka na hali hii.
Upweke unatajwa kuwa ni hali inayoweza kusabaisha kifo kwani hupelekea kuongezeka kwa viwango vya homoni za mkazo yaani ‘stress’, kuvimba, kuharibu mifumo ya kinga za mwili pamoja na kuvuruga mifumo ya kulala mwilini na hii huwaweka watu katika hatari ya kuugua magonjwa makubwa na kupata majeraha yanayo hatarisha maisha.
Imeelezwa kuwa vifo vya umri mdogo hupungua kwa asilimia 50 endapo watu watakua wanaishi kwa tabia ya mwingiliano katika jamii yaani ‘social interaction’ na kwamba upweke huu pia unachangiwa na ongezeko la watu kuishi peke yao na kuongezeka kwa matumizi ya smartphones na mitandao ya kijamii.
Uliikosa hii? “Sisi tulimtambua kama House girl na sio Mama yetu” – Mtoto wa Marehemu